Jumanne 7 Oktoba 2025 - 16:33
Mikusanyiko na shughuli za kitamaduni za kuunga mkono Palestina yafanyika nchini Argentina

Hawza/ Makundi na mashirika mbalimbali mjini Buenos Aires yamefanya mikusanyiko, vipindi vya redio na shughuli za kitamaduni ili kuonesha uungaji wao mkono watu wa Palestina na kutangaza upinzani wao dhidi ya ushiriki wa kimataifa katika mgogoro wa Palestina. Moja ya mikusanyiko muhimu zaidi itafanyika siku ya Jumanne tarehe 7 Oktoba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika kukaribia kwa mkusanyiko mkubwa wa kuunga mkono watu wa Palestina utakaofanyika tarehe 7 Oktoba, shughuli mbalimbali zimepangwa na kutekelezwa nchini Argentina. Kamati ya Mshikamano ya Argentina na Watu wa Palestina ilifanya kipindi cha redio mbele ya Wizara ya Mambo ya Nje (Esmeralda 1212). Kipindi hiki kilibeba kaulimbiu isemayo “Sio kwa jina letu” kikieleza upinzani wake dhidi ya mkutano wa viongozi na Netanyahu, na kilitoa wito wa kukatisha uhusiano na Israel pamoja na kuunga mkono msafara wa kimataifa wa “Sumud”.

Kundi la “Wapenda Mabadiliko wa Kipalestina” (Palestinos Autoconvocados) pia lilifanya mkusanyiko mbele ya Obelisco (Uwanja wa Jamhuri) kuonesha upinzani wake dhidi ya kura turufu (veto) ya Marekani katika Umoja wa Mataifa na kutoidhinishwa kwa azimio la kusitisha mapigano. Walisisitiza kuwa nguvu ya kura turufu ya baadhi ya nchi inapuuzia matakwa ya wengi.

Kadhalika, makundi kadhaa ya wenyeji, yakishiriki “Mkutano kwa ajili ya Palestina huko Vicente López”, yalitoa wito wa kukusanyika mbele ya Ikulu ya Rais huko Olivos ili kuonesha ishara ya mshikamano.

Mbali na mikusanyiko hii, hatua za vitendo za kusaidia familia za Kipalestina huko Ghaza pia zinaendelea. Miongoni mwazo ni kusaidia familia ya Abdullah Al-Tayebi, mkazi wa Buenos Aires, ambayo familia yake inahitaji kuhamishiwa kusini mwa Ukanda wa Ghaza kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Israel. Aidha, kampeni za kijamii kama “Kufuma kwa ajili ya Mshikamano na Gaza”, “Meza kwa ajili ya Palestina” na “Ndege elfu moja kwa ajili ya Gaza” zinaendelea, na zinatoa msaada wa moja kwa moja wa kusaidia familia za Kipalestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha